Katika hali ya dharura ya papo hapo, inayotishia maisha kama vile:
- Maumivu ya kifua au kubanwa kwa kifua
- Ganzi ya ghafla au kupooza kwa uso, mkono au mguu
- Kuchomeka kwingi
- Ajali mbaya
- Kutokwa na damu nyingi
- Ugumu wa kupumua
- Maumivu makali
- Kukosa fahamu
Piga simu kwa Ziro Tatu (000) na mpokea simu ataweza kukusaidia .

Ikiwa unahitaji huduma ya haraka lakini sio hatari kwa maisha:

Tembelea Kliniki ya Huduma ya Haraka
Huduma ya bure, hakuna rufaa au kadi ya matibabu inahitajika

Pia simu ya Video kwa Mtandao wa ED
Huduma ya bure ya masaa 24/7, hakuna rufaa au kadi ya matibabu inahitajika
Unaweza pia kupata usaidizi kutoka kwa:

Muuguzi wa Kwenye Simu
24/7 piga 1300 60 60 24

Daktari wako wa mahali
Piga 13SICK (13 7425)

Mfamasia wa eneo lako
Tafuta mtandaoni ili kupata duka la dawa karibu
Updated